Idadi ya vifo vilivyotokana na vurugu nchini Madagascar yafikia 19
2022-08-31 08:45:52| cri


 

Jeshi la Polisi nchini Madagascar jana limethibitisha kuwa, mapigano kati ya askari polisi na waandamanaji yaliyotokea Ikongo, kusini mashariki mwa nchi hiyo, yamesababisha vifo vya watu 19 na wengine 21 kujeruhiwa.

Karibu watu 100 walivamia kituo cha polisi cha Ikongo Jumatatu asubuhi kudai watu wanne ambao walikuwa wakishikiliwa kwa tuhuma za kumteka nyara mtoto mwenye ulemavu wa ngozi. Lakini polisi walikataa kutekeleza madai hayo, hivyo watu hao waliamua kuvamia kwa nguvu kituo hicho na polisi kujibu hatua hiyo.