UM wasema walinzi wa amani wapeleka dawa mkoani Gao nchini Mali licha ya magaidi kufunga njia kuu ya usafirishaji
2022-09-01 08:33:43| CRI

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema, walinzi wa amani wa Umoja huo nchini Mali wanabeba dawa muhimu na kuzipeleka katika ghala mjini Gao kutokana na magaidi wenye silaha kufunga njia muhimu ya usafirishaji kuanzia mwezi Mei mwaka huu.

Amesema askari hao watapeleka tani 1.5 ya dawa muhimu mjini Gao kila wiki, na kuongeza kuwa hatua hiyo inafuatia ombi lililotolewa na mamlaka za kanda hiyo zinazofanya kazi kukabiliana na athari za uhaba wa dawa.

Amesema Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Mali pia kinatoa msaada katika mji wa Douentza, ambako walinzi wa amani kutoka Togo wanatoa matibabu kwa familia 450 kupitia kliniki inayotembea.