Rais wa China apongeza Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China 2022
2022-09-01 08:29:11| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China ya Mwaka 2022 yaliyofunguliwa jana Agosti 31 na yatafanyika hadi Septemba 5 hapa Beijing.

Kwenye barua yake, rais Xi amesema maonesho hayo ni jukwaa muhimu la China katika kufungua mlango zaidi, kuzidisha ushirikiano na kuhimiza uvumbuzi, na yametoa mchango chanya kwa kuhimiza maendeleo ya sekta ya huduma na biashara ya huduma duniani.

Rais Xi amesisitiza kuwa, kwa kushikilia utaratibu halisi wa pande nyingi, ujumuishi na mafanikio ya pamoja, China inapenda kushirikiana na nchi nyingine duniani kuhimiza uchumi wa huduma unaofungua mlango, ili kutia nguvu kwa ufufukaji na maendeleo ya uchumi wa dunia.