Wanaanga wa China walioshiriki kwenye safari ya chombo cha anga za juu cha Shenzhou-14 watoka nje ya kituo cha anga cha China
2022-09-01 21:02:08| CRI

Wanaanga wa China walioshiriki kwenye safari ya chombo cha anga za juu cha Shenzhou-14 wametoka nje ya kituo cha anga za juu cha China leo tarehe mosi Septemba kwa mara yao ya kwanza tangu wawasili kituoni humo mwezi Juni mwaka huu.

Saa kumi na mbili na dakika 26 leo jioni kwa saa za Beijng, mwanaanga Chen Dong alifungua mlango wa kutoka nje wa moduli ya maabara ya Wentian na saa moja na dakika 9 jioni akafanikiwa kutoka nje ya kituo hicho pamoja na mwenzake Liu Yang huku mwanaanga mwingine Cai Xuzhe akifanya kazi ndani ya kituo kuwasaidia wenzake pale nje.