Sudan yaonya dhidi ya kuongezeka kwa kina cha maji ya Mto Nile
2022-09-01 08:32:39| CRI

Mamlaka nchini Sudan zimesema kina cha maji katika Mto Nile kinaongezeka kwa kasi katika sehemu ya mto huo nchini Sudan na kusababisha wasiwasi wa kutokea mafuriko katika maeneo ambayo tayari yamekumbwa na maji yaliyotokana na mafuriko ama kuathirika na mvua kubwa zinazonyesha kuanzia mwezi Juni.

Wizara ya Rasilimali ya Maji na Umwagiliaji nchini humo imetoa taarifa ikisema, sehemu zote za Mto Blue Nile, tawi kubwa la Mto Nile, zinashuhudia kuongezeka kwa kina cha maji na kukaribia ngazi ya mafuriko, na kuongeza kuwa, kina cha maji katika Mto Nile kimefikia mita 16.58, ambacho ni cha juu zaidi katika majira haya ya mwaka.

Mtaalamu wa mazingira na hali ya hewa nchini humo Mahjoub Hassan amesema, nchi hiyo haikujiandaa kwa mvua kubwa kutokana na miundombinu dhaifu, na kuongeza kuwa, hali inazidi kuwa mbaya kutokana na ukosefu wa mitaro ya kupitishia maji ya mvua.