Mapigano kaskazini mwa Ethiopia yasababisha watu kukimbia makazi yao
2022-09-02 08:35:20| CRI

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema, mapigano katika eneo la kaskazini mwa Ethiopia yamesababisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao, na kuleta changamoto katika utoaji wa misaada ya kibinadamu.

Amesema Umoja huo pamoja na wenzi wake wanaendelea kutoa misaada katika eneo la kaskazini mwa Ethiopia, ikiwemo mkoa wa Afar ambako zaidi ya watu 31,000 wamepokea msaada wa chakula, na watu zaidi ya 8,000 wamepata huduma za afya kuanzia Agosti 24.

Hata hivyo, Dujarric amesema, pamoja na kwamba ndege za misaada za Umoja huo zimeshindwa kuingia katika mkoa wa Tigray, na njia kuu inayoingia Mekelle kushindwa kupitika, wafanyakazi wa mashirika ya kibinadamu wametoa msaada wa malori 17 ya mbolea wiki hii ili kuwasaidia wakulima katika kanda hiyo wakati huu wa msimu wa kilimo.

Ameongeza kuwa, zuio hilo limeshindwa kuwafanya wahudumu wa mashirika ya kibinadamu kutoa msaada wa chakula kwa zaidi ya watu 39,000 katika Ukanda wa Kaskazini Magharibi mkoani Tigray.