Umoja wa Afrika wasema amani na hali ya usalama vimeimarika barani Afrika
2022-09-02 08:30:56| cri


Kaimu mkuu wa Idara ya Ukusanyaji silaha, Kuondoa makundi na Kurejesha katika jamii, na Mageuzi ya sekta ya Usalama katika Umoja wa Afrika (AU) Bw. Christopher Suna Kayoshe amesema, hali ya amani na usalama katika bara hilo inaimarika kutokana na juhudi za pamoja za kupunguza migogoro ya kitaifa na kimataifa.

Bw. Kayoshe pia amesema, taasisi dhaifu za mitaa, pamoja na umaskini na kushuka kwa uchumi, ni sababu za pamoja za ukosefu wa amani na usalama barani humo.