Serikali ya Ethiopia yalaani kundi la waasi kwa kufanya mashamblizi mapya
2022-09-02 08:11:49| cri


 

Serikali ya Ethiopia jana imelilaani kundi la Harakati za Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF) kwa kufanya mashambulizi mapya kwenye maeneo tofauti.

Katika taarifa yake, Idara ya Mawasiliano ya serikali ya Ethiopia imesema, kundi la TPLF limefanya mashambulizi mapya kwenye maeneo tofauti katika mkoa wa Amhara ulio jirani na mkoa wa Tigray.

Taarifa hiyo pia imeitaka jumuiya ya kimataifa iweke shinikizo zaidi dhidi ya kundi la TPLF, kwa ajili ya usuluhishi wa kiamani wa mgogoro.