Kitendo cha Marekani kudai kuwa China inaibebesha Afrika mzigo wa madeni kinaendana na mawazo ya Vita Baridi
2022-09-02 08:33:46| CRI

Mchambuzi kutoka Kituo cha Sera za Nishati cha Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani, Harry Verhoeven amesema, kitendo cha Marekani kuipaka matope China kwa madai kuwa inaiongezea Afrika mzigo wa madeni kinaakisi mtazamo wake wa Vita Baridi.

Verhoen amesema, Marekani tayari inaandaa jukwaa la kisomo ambalo linatakiwa kuitambua China kama nchi pekee inayowajibika na mlundiko wa madeni kwa Afrika, na kulikamata bara hilo katika mtego wa madeni.

Ameongeza kuwa, ni wakopeshaji kutoka nchi za Magharibi ambapo wamechukua nafasi kubwa katika ongezeko la madeni kwa nchi za Afrika.

Wakati huohuo, Bw. Verhoen ameeleza uwekezaji wa China barani Afrika kuwa ni wa muhimu sana, akisema kuwa watu wachache katika bara hilo ambao watapinga nafasi muhimu iliyochukuliwa na China katika suala hilo.