Mauzo ya Kenya kwa nchi za Afrika yameongezeka kwa asilimia 25 katika nusu ya kwanza mwaka huu
2022-09-02 08:36:21| CRI

Benki Kuu ya Kenya (CBK)imetoa ripoti ikisema, mauzo ya Kenya kwa nchi nyingine za Afrika yameongezeka kwa asilimia 25 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2022, huku ikikabiliwa na athari kutokana na mgogoro kati ya Russia na Ukraine.

Benki hiyo imesema mauzo ya nje yaliongezeka hadi shilingi bilioni 130.05, sawa na dola za kimarekani bilioni 1.09 kutoka dola za kimarekani milioni 865 katika kipindi kama hicho mwaka 2021.

Mauzo mengi ya Kenya yalikwenda Afrika Kusini na Tanzania yakipita yale ya Uganda, ambayo ni mshirika mkubwa zaidi wa biashara wa nchi hiyo kwa miaka mingi.

Nchi nyingine zinazoongoza kwa mauzo ya nje ya Kenya ni Zambia, Zimbabwe, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Somalia.