Waangalizi wa amani wa Sudan Kusini waidhinisha kuongeza muda wa serikali ya mpito
2022-09-02 08:35:58| CRI


 

Waangalizi wa amani nchini Sudan Kusini wamepiga kura na kukubali kuongeza muda wa serikali ya mpito ya nchi hiyo kwa miaka miwili.

Mwenyekiti wa muda wa Tume ya Pamoja ya Ufuatiliaji na Tathmini (R-JMEC) Charles Tai Gituai amesema, theluthi mbili ya wajumbe wa tume hiyo waliopiga kura waliidhinisha hatua hiyo kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa katika Makubaliano ya Ustawi yanayolenga kumaliza migogoro nchini Sudan Kusini.

Miongoni mwa wajumbe ambao hawakupiga kura ni pamoja na wajumbe kutoka Marekani, Uingereza na Norway, ambao wanataka mazungumzo ya miezi mitatu kabla ya kuongeza muda wa serikali ya mpito.

Gituai amesema, hivi sasa kuongezwa kwa muda wa serikali kutahitaji kuidhinishwa na bunge la mpito.