Mtaalamu wa Afrika atoa wito wa hatua za uvumbuzi ili kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza
2022-09-02 08:34:33| CRI

Mkuu wa Mtandao wa Kudhibiti Umasikini na Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Kanda ya Afrika Magharibi Emmanuel Mensah amesema, serikali, wafadhili na sekta husika zinapaswa kutunga mikakati thabiti ili kukabiliana na kuongezeka kwa vifo vinavyotokana na magonjwa yasiyoambukiza barani Afrika.

Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, Afrika ilikuwa katika nafasi nzuri ya kupunguza mzigo wa magonjwa ya saratani, kisukari, shinikizo la damu na maambukizi sugu katika mfumo wa hewa pindi serikali zitakapotoa kipaumbele kwenye elimu, mafunzo kwa wafanyakazi wa afya, uwekezaji na maabara pamoja na usimamizi wa kesi husika.

Takwimu kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa, magonjwa yasiyoambukiza kama saratani, kisukari na magonjwa ya moto yamesababisha asilimia 37 ya vifo katika kanda ya Sahara barani Afrika mwaka 2019, ikiwa ni ongezeko la asilimia 24 ikilinganishwa na mwaka 2000.