Watu watano wamefariki kwenye machimbo ya mawe nchini Uganda
2022-09-05 08:58:30| CRI

Watu watano wamefariki dunia kwenye ajali ya kuporomoka kwa machimbo ya mawe iliyotokea jumamosi katika wilaya ya Wakiso katikati ya Uganda.

Taarifa iliyotolewa na polisi imesema miili ya watu watano imetolewa kwenye kifusi, na kati ya waliokufa wanne walikuwa ni wafanyakazi vibarua, na mmoja alikuwa ni dereva wa lori.

Taarifa iliyotolewa na polisi inasema uchunguzi wa chanzo cha ajali unaendelea, na wameshauri watu wa maeneo ya karibu kutosogelea eneo la machimbo kutokana  na hatari ya usalama kwa maisha yao.

Ajali nyingine kama hiyo ilitokea mwezi juni mwaka jana na kusababisha vifo vya watu wanne, baada ya machimbo ya mawe kuporomoka mjini Kampala.