Rais mteule wa Kenya aahidi kufufua uchumi na kuleta mshikamano
2022-09-06 08:55:03| CRI

Rais mteule wa Kenya Bw. William Ruto amesema serikali yake itatoa kipaumbele kwenye kuleta mageuzi ya uchumi, amani, mapatano na mshikamano baada ya kuapishwa kuwa Rais wiki ijayo.

Bw. Ruto alisema hayo wakati akiongea kwa njia ya televisheni baada ya mahakama kuu ya Kenya kutangaza kuwa alichaguliwa kihalali kuwa rais wa tano wa Kenya. Bw. Ruto amesema safari ya kuleta mageuzi ya uchumi wa Kenya na kufungua fursa za uchumi kwa kila mtu bila kujali kabila, rangi, jinsia au chama, imeanza.

Mahakama kuu ya Kenya imemthibitisha Bw. Ruto kuwa mshindi wa uchaguzi wa Kenya, baada ya kusema pingamizi dhidi ya ushindi wake lililowekwa na mpinzani wake Bw. Raila Odinga na asasi za kijamii, kutupiliwa mbali na mahakama kwa kukosa ushahidi.