Spika wa bunge la China atoa mwito wa kuimarisha mabadilishano ndani ya mfumo wa BRICS
2022-09-07 08:52:29| CRI

Spika wa bunge la umma la China Bw. Li Zhanshu ametoa mwito kwa mabunge ya nchi za BRICS (Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini) kutoa mchango zaidi katika kuimarisha mshikamano na ushirikiano kati ya nchi za kundi hilo.

Akiongea kwenye mkutano wa mabunge ya nchi za BRICS uliofanyika kwa njia ya video na kushirikisha wabunge waandamizi kutoka nchi za kundi hilo, Bw. Li amesema mabadilishano ya kirafiki kati ya mabunge, yanatoa uhakikisho wa kisheria na uungaji mkono wa kisera kwenye ushirikiano kati ya nchi za BRICS.

Pia amesema bunge la China liko tayari kuimarisha ushirikiano na mabunge ya nchi za BRICS, ili kuhimiza ushirikiano kwenye maendeleo na kutoa mchango katika kufufua uchumi na maendeleo endelevu ya dunia.