Katibu mkuu wa UM alaani shambulizi nchini Burkina Faso lililosababisha vifo vya raia 35
2022-09-07 09:12:44| CRI

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amelaani vikali shambulizi la mabomu lililotokea Jumatatu wiki hii kati ya miji ya Djibo na Bourzanga, kaskazini mwa Burkina Faso, na kusababisha vifo vya raia wasiopungua 35 na wengine 37 kujeruhiwa.

Taarifa iliyotolewa na mamlaka za huko imesema shambulizi hilo lilitokea wakati lori moja la msafara uliosindikizwa kuelekea mjini Ouagadougou lilipokanyaga bomu lililotengenezwa kienyeji.

Bw. Guterres alitoa salamu za rambirambi kwa familia za wahanga na watu wa Burkina Faso, na amezitaka mamlaka za nchi hiyo kuwatafuta wahusika wa shambulizi hilo na kuwafikisha mbele ya sheria. Pia amesisitiza kuwa UM utaendelea kushirikiana na Burkina Faso na nchi washirika duniani katika juhudi za kulinda raia, kukabiliana na changamoto za kibinadamu na kuhimiza amani na ustawi wa kudumu.