Wanafunzi wa Namibia wafurahia sherehe za Sikukuu ya Mbalamwezi ya jadi ya China
2022-09-08 08:37:49| CRI

Wanafunzi wa  Chuo cha Confucius katika Chuo kikuu cha Namibia (UNAM) wamefurahia shughuli mbalimbali za kiutamaduni za kusherehekea Sikukuu ya Mbalamwezi ya jadi ya China inayowadia Ijumaa Septemba 10.

Mkurugenzi wa  chuo hicho katika Chuo kikuu cha Namibia Bw. Liu Dianbo amesema ili kuimarisha zaidi mawasiliano ya kiutamaduni na kilugha  katika chuo chake, kuna haja ya kuwafahamisha wanafunzi kuhusu moja ya sikukuu muhimu zaidi  katika utamaduni wa China na undani wake.

Kwenye shughuli hizo, wanafunzi wa chuo hicho walionja keki ya mbalamwezi , kushiriki kwenye  maonesho ya michezo ya Sanaa ya China, na kuwasiliana na wahadhiri kupitia kuimba nyimbo, kusoma mashairi na kujibu maswali kwa lugha ya  Kichina.