Wanaanga wa China wanaongea na wanafunzi wa Tanzania kutoka anga ya juu
2022-09-08 08:53:01| CRI

Wanaanga watatu wa China wameongea na wanafunzi wa Tanzania kwa njia ya video moja kwa moja kutoka kwenye anga ya juu, katika shughuli iliyoandaliwa na ubalozi wa China nchini Tanzania.

Wanaanga hao watatu walio kwenye chombo cha anga ya juu cha China Shenzhou, walikuwa na wakati wa maswali na majibu kutoka shule za sekondari Benjamin William Mkapa na Zanaki za mjini Dar es salaam.

Kwenye shughuli hiyo wanafunzi wa Tanzania walikuwa na udadisi mkubwa kuhusu maisha na kazi za wanasayansi hao kwenye anga ya juu.

Naibu Katibu mkuu wa wizara ya Elimu, Sayansi na Utamaduni Bw. James Mdoe amesema Tanzania inaufanyia mabadiliko mtaala wa elimu ili kuhimiza ufundishaji wa masomo ya sayansi.

Balozi wa China nchini Tanzania Bibi Chen Mingjian amesema China na Tanzania zina fursa kubwa ya ushirikiano kwenye sekta ya utafiti wa anga ya juu, na amewahimiza vijana zaidi kujifunza sayansi.