Rais wa China atuma barua ya pongezi kwa mkutano wa taifa wa maendeleo ya viwanda maalum na vya kisasa vidogo na vya kati
2022-09-09 15:15:35| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa mkutano wa taifa wa maendeleo ya viwanda vidogo na vya ukubwa wa kati ambavyo ni maalum na vya kisasa unaofanyika Nanjing, mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China.

Katika barua yake, rais Xi ameeleza kuwa viwanda vidogo na vya ukubwa wa kati ni muhimu kwa kila kaya, na vimekuwa nguvu muhimu ya kuendeleza uvumbuzi, kuwezesha upatikanaji wa ajira na kuboresha maisha ya watu.

Amesema anatumai kuwa viwanda hivyo maalum na vya kisasa vinavyozalisha bidhaa mpya na za kipekee vinaweza kujikita katika kuboresha biashara zao kuu ili kuchukua nafasi ya muhimu zaidi katika kutuliza minyororo ya viwanda na ugavi na kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, amezitaka kamati za Chama na serikali katika ngazi zote kutekeleza kihalisi maamuzi na mipangilio ya Kamati hiyo na kujenga mazingira mazuri kwa maendeleo ya viwanda vidogo na vya ukubwa wa kati.