Hadithi ya Xi Jinping na walimu wake
2022-09-09 15:20:01| cri

"Nina walimu wengi ambao wamenifundisha, na bado ninakumbuka sura zao. Walinifundisha ujuzi na maadili, ambazo zimenifaidisha sana ... "

Hivi ndivyo Xi Jinping, kiongozi mkuu wa China, aliwahi kusema wakati alipokuwa akishukuru kwa walimu wake. Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, Xi Jinping ameingia mara nyingi katika kampasi na madarasa ili kuwasiliana na walimu na wanafunzi. Alisema kuwa mpango wa karne nzima umezingtia zaidi elimu; na mpango wa elimu umezingatia walimu. Kutokana na maneno haya, si vigumu kuona kwamba, katika mawazo ya Xi Jinping, elimu daima imekuwa kipaumbele cha maendeleo. Katika maadhimisho ya miaka 38 ya Siku ya Walimu ya China ya mwaka 2022, wacha tujifunze pamoja "Hadithi ya Xi Jinping na Walimu wake".

Mwalimu wa Kichina Chen Qiuying: Heshima yake kwa walimu haiwezi kusahaulika

Mwezi Septemba mwaka 1965, Chen Qiuying, mwalimu wa Kichina wa sekondari ya chini mwaka wa kwanza, alikaribisha darasa jipya la wanafunzi, akiwemo Xi Jinping mwenye umri wa miaka 12.

Darasani, Xi Jinping ana umri mdogo kuliko wengine. Mwalimu Chen aligundua kuwa kijana huyu ambaye hapigani mara kwa mara na wanafunzi wenzake wakati wa mapumziko ana tabia njema na ya ukarimu. Chen Qiuying alifundisha mashairi ya mshairi Du Fu wa Enzi ya Tang. Mashairi mengi yaliyoandikwa na mshairi huyu yamejaa huruma na upendo kwa watu wa kawaida. Mwalimu Chen alikumbuka kwamba baada ya kumaliza kufundisha mashairi ya Du Fu, Xi Jinping alimfuata mwalimu baada ya darasa, akisema kwamba anampenda Du Fu, mshairi mkubwa, na kutarajia kusoma zaidi kazi za Du Fu. Kijana mwenye bidii na mtazamo mkubwa aliacha hisia kubwa kwa Bw. Chen.

Mwaka 1999, Chen Qiuying, ambaye alikuwa ameshastaafu, alifanya kazi bila kuchoka kutengeneza na kuchapisha mkusanyiko wa hadithi za paukwa pakawa zenye maneno zaidi ya 100,000. Alituma kitabu chake kipya kwa Xi Jinping. Muda mfupi tu baada ya kitabu hicho kutumwa, Xi Jinping, aliyekuwa naibu katibu wa Kamati ya Chama ya Mkoa wa Fujian na kaimu gavana wa mkoa, alimjibu. Chen Qiuying alisema katika barua yake ya majibu Xi Jinping alitumia neno "heshima kwa walimu na ualimu", na neno "heshima" linaonyesha urafiki kati ya wanafunzi na walimu.

Miaka sita iliyopita, katika mkesha wa Siku ya Walimu iliyokuwa Septemba 9, 2016, Xi Jinping, ambaye alikuwa tayari ni kiongozi mkuu wa China, alirejea katika shule yake ya zamani, ya Bayi ya Beijing, na kuwatembelea walimu na wanafunzi. Siku hiyo hiyo, Xi Jinping alikutana na Chen Qiuying na walimu wengine kadhaa waliokuwa wamemfundisha. Alipomsikia Xi Jinping akisema kwamba shule yake ya zamani ndio mahali penye mizizi na upendo wake, hakuna mkuu hapa, sote ni wanafunzi tu, Chen Qiuying mwenye umri wa miaka 77 alisema kidogo atokwe na machozi. Baada ya miongo kadhaa, urafiki wao baina ya mwalimu na mwanafunzi haujabadilika hata kidogo. 

Katika Shule ya Bayi, mwalimu mzee alimwambia Katibu Mkuu Xi Jinping: "Umewaletea watu furaha." Xi Jinping alijibu: "Ni mwalimu aliyetufunza."

Mwalimu Chen Zhonghan aliwahi kuwa naibu mwalimu mkuu wa Xi Jinping. Alipokutana na Xi Jinping mjini Beijing mwaka 2016, Chen Zhonghan alimwambia Xi Jinping, natumai utaweza kuiongoza nchi vizuri zaidi na kupata maendeleo makubwa katika nyanja zote. Xi Jinping alisema: "Asante kwa kuniamini, nitaiweka moyoni mwangu." Mwalimu Chen alisema kwamba neno "kuniamini" lilimgusa sana moyoni. Alitoa maoni yake kuhusu Xi Jinping: "Katika miaka hii, haijalishi ni wadhifa gani, huwa anatukumbuka sisi walimu ambao tumemfundisha. Ni mtu wa fadhila na upendo."

Baada ya kuhitimu Shule ya Bayi, Xi Jinping alikwenda Kijiji cha Liangjiahe, Yan'an, mkoani Shaanxi. Katika miongo kadhaa tangu hapo, Xi Jinping amekuwa akikumbuka shule yake ya zamani na walimu wake. Xi Jinping alipokuwa akifanya kazi katika maeneo mengine, kila alipokuja Beijing, kila mara alijitahidi awezavyo kutenga muda wa kuwatembelea walimu waliomfundisha masomo yake na kumuondolea mashaka yake. Xi Jinping amesisitiza mara kwa mara kwamba ualimu unapaswa kuwa taaluma inayoheshimika na kuonewa wivu kwelikweli katika jamii, na kujenga mwelekeo mzuri wa kuheshimu walimu na ualimu katika jamii nzima.