Xi Jinping na mwenyekiti wa AU wapeana pongezi za maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Umoja huo na uhusiano kati ya China na AU
2022-09-09 14:55:38| CRI

Rais Xi Jinping wa China na mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika, ambaye pia ni rais wa Senegal Macky Sall leo wamepeana barua za pongezi za maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika na uhusiano kati ya China na Umoja huo.

Rais Xi amesema, katika miaka 20 iliyopita, Umoja wa Afrika umeongoza nchi za Afrika kupiga hatua kwa kushirikiana kujiendeleza, kustawisha na kujenga utandawazi wa kiviwanda, na kuonyesha nguvu za Afrika katika mapambano dhidi ya COVID-19, kulinda hali yenye pande nyingi na maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea. Uhusiano kati ya China na Umoja wa Afrika umeonesha umuhimu mkubwa katika kurithi urafiki wa jadi kati ya China na Afrika na kuimarisha mshikamano na ushirikiano katika zama mpya.

Rais Xi amesema anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Umoja wa Afrika na anapenda kushirikiana na rais Sall na viongozi wengine wa nchi wanachama wa AU kutekeleza kwa pamoja matokeo ya mkutano wa 8 wa mawaziri wa baraza la FOCAC, kuungana mkono katika masuala makubwa yanayofuatiliwa na pande zote mbili, na kuimarisha uwakilishi na sauti ya nchi zinazoendelea kuhusu mambo ya kimataifa, ili kutoa mpango mpya kwa ajili ya kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Afrika katika zama mpya.

Kwa upande wake, Rais Sall amepongeza sana urafiki wa jadi kati ya Afrika na China, ushirikiano wa kushikamana, na uhusiano wa kiwenzi wenye uhai chini ya baraza la FOCAC, pia amesisitiza kuwa Afrika inashikilia kuunga mkono sera ya kuwepo kwa China moja na kuunga mkono kujenga kwa pamoja jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Afrika.