Rais Xi ajibu barua kutoka wanafunzi wa programu ya mafunzo ya walimu katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Beijing
2022-09-09 09:11:36| CRI

Rais Xi Jinping wa China amejibu barua aliyoandikiwa na wanafunzi wanaoshiriki kwenye programu ya mafunzo ya walimu katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Beijing, inayolenga kutoa mafunzo kwa walimu watakaotoa huduma katika maeneo yaliyoko nyuma kimaendeleo kote nchini, kabla ya Siku ya Walimu ya China inayoadhimishwa Septemba 10 kila mwaka.

Kwenye barua yake, Rais Xi amesema anafurahia kufahamu kuwa, wanafunzi hao kupitia masomo ya darasani na mazoezi ya ufundishaji katika mwaka wa kwanza wa shule, wameongeza ujuzi, kupanua upeo wao, na kuimarisha dhamira yao ya kufundisha na kuelimisha watu mashinani.

Rais Xi amewataka wanafunzi hao kujitahidi kuwa walimu wanaokiridhisha Chama na wananchi, na kusaidia kuandaa kizazi kipya cha vijana wenye vipaji, maadili mema, afya ya kimwili, uwezo wa kutambua uzuri na ustadi wa kutenda kazi unaohitajika kuendeleza shughuli kubwa ya usoshalisti.