Malkia Elizabeth II wa Uingereza afariki dunia akiwa na miaka 96
2022-09-09 08:53:03| CRI

Kasri la Buckingham limetangaza kuwa Malkia Elizabeth II wa Uingereza amefariki dunia jana mchana akiwa na umri wa miaka 96. Malkia amefariki dunia siku moja baada ya kasri hilo kutangaza kuwa Malkia alikuwa chini ya uangalizi mkali wa madaktari kutokana na wasiwasi kuhusu afya yake.

Katika siku za karibuni Malkia alikuwa na matatizo ya kutembea baada kupona COVID-19 mwezi Februari. Kifo chake pia kimetokea siku mbili baada ya kumteua Liz Truss kuwa waziri mkuu mpya wa Uingereza.

Kasri la Buckingham pia limetangaza kuwa mtoto wa Malkia mwanamfalme Charles kuwa mfalme mpya.

Kwa mujibu wa mfumo wa kifalme wa Uingereza, Malkia akifa taji linaenda kwa mtoto wake mkubwa. Bado haijulikani kama kutakuwa na sherehe rasmi ya Mfalme Charles kutawazwa.