Wajasiriamali wanawake kwenye sekta ya kilimo Afrika wapewa tuzo kwenye baraza la kilimo Rwanda
2022-09-09 08:53:44| CRI

Wajasiriamali wanawake kwenye sekta ya kilimo kutoka Gambia, Rwanda, Benin na Nigeria wameibuka washindi wa tuzo yenye thamani ya dola elfu 85, iliyotolewa kwa wajasiriamali wanawake kwa mwaka huu mjini Kigali.

Shirikisho la mageuzi ya kilimo barani Afrika AGRA limetangaza tuzo hiyo kwenye mkutano wa kilele wa mageuzi ya kilimo unaoendelea mjini Kigali.

Washindi hao walioteuliwa katika bara zima, waliteuliwa katika makundi ya mjasiriamali wa kilimo mwanamke, mvumbuzi wa teknolojia za kilimo mwanamke, mjasiriamali wa kampuni iliyoongeza thamani, na tuzo ya jumla.

Mkuu wa Agra Bibi Agnes Kalibata amesema washindi hao wote ni mfano wa kuigwa kwa maelfu ya wanawake wanaofanya kazi kwenye sekta ya kilimo barani Afrika.