Bwawa la uchimbaji madini nchini Afrika Kusini lapasuka na kusababisha vifo vya watu watatu
2022-09-12 08:39:55| CRI

Bwawa la kuchimba madini lililoko katikati mwa Afrika Kusini lilipasuka jana asubuhi kwa saa za huko na kusababisha mafuriko ambayo yamesomba nyumba na kuharibu miundo mbinu na hadi sasa watu watatu wamefariki na wengine 40 kujeruhiwa.

Msemaji wa idara ya Utawala wa Ushirika na Mambo ya jadi ya nchi hiyo CoGTA Lungi Mtshali amesema, serikali imetuma idara mbalimbali huko Jagersfontein, katika jimbo la Free State, zikiwemo timu ya matibabu ya dharura ya polisi, idara ya afya, idara ya usimamizi wa maafa, idara ya jamii, watu wa uokoaji na wahandisi.