Waziri: Misri ni moja ya nchi zilizoathirika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi
2022-09-12 08:28:52| CRI

Waziri wa Rasilimali Maji na Umwagiliaji wa Misri, Hani Suweilam amesema Misri ni moja ya nchi zilizoathirika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi duniani.

Hayo ameyasema wakati wa ufunguzi wa kongamano la mazingira na maendeleo wakati nchi hiyo ikiwa kwenye maandalizi ya kuandaa mkutano wa 27 wa Umoja wa Matifa kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi (COP27) unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba huko Red Sea resort mjini Sharm El-Sheikh. Amebainisha kuwa Misri inateseka na uhaba wa maji, joto kali, mmomonyoko wa udongo na maji ya chumvi kuingia kwenye maji baridi.

Waziri Suweilam pia amezitaka nchi zote kuzidisha ushirikiano katika kushughulikia hali ya hewa kali na kusisitiza haja ya kuweka sekta ya maji, chakula na kilimo kwenye ajenda ya hali ya hewa duniani.