Tanzania yapanga kujenga makumbusho kubwa ya marais
2022-09-12 08:29:32| CRI

Tanzania inapanga kujenga makumbusho kubwa ya marais katika mji mkuu wake Dodoma ili kukuza uelewa wa masuala mbalimbali yanayowahusu marais.

Hayo yamesemwa jana Jumapili na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Kale katika Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Kristowaja Ntandu. Amebainisha kuwa makumbusho hayo yatatumika kama hifadhi ya nyaraka, rikodi, na vitu vya kuhistoria vya marais wa nchi hiyo. Kwa sasa maandalizi yanaendelea ikiwemo michoro ya ramani ya makumbusho na ukusanyaji wa taarifa muhimu za marais.

Dkt. Ntandu pia ameeleza kuwa waziri wa Maliasili na Utalii, Pindi Chana Jumamosi alikagua maandalizi ya ujenzi wa makumbusho hayo katika eneo la Chisichili ambalo lina ukubwa wa hekta 20, na kwamba baada ya makumbusha hayo kujengwa yataongeza idadi ya vivutio vya utalii. Tanzania imeongozwa na marais sita tangu ijipatie uhuru wake.