Uchumi wa Kenya watarajiwa kukua kwa asilimia 5.8 katika mwaka wa fedha wa 2022/23
2022-09-15 09:38:29| CRI

Wizara ya Fedha ya Kenya imekadiria kuwa uchumi wa nchi hiyo utakua kwa asilimia 5.8 katika mwaka wa fedha wa 2022/23.

Kwenye waraka wake wa mapitio ya bajeti na matarajio ya 2022 uliotolewa Jumatano, Wizara hiyo imesema ukuaji huo utasaidiwa na kuongezeka kwa shughuli za sekta binafsi, ikiwa ni pamoja na kufufuka kwa sekta ya kilimo,

Imeeleza kuwa makaridio haya yataimarishwa na utekelezaji unaoendelea wa vipaumbele vya kimkakati vya serikali chini ya Ajenda ya 'Big Four' na mkakati wa kufufua uchumi. Zaidi ya hayo, serikali inatekeleza awamu ya tatu ya mipango ya uhamasishaji wa kiuchumi inayolenga mikakati ya kukwamua kilimo, afya, elimu, kukabiliana na ukame, sera, miundombinu, ushirikishwaji wa fedha, nishati na uhifadhi wa mazingira.

Hata hivyo, Wizara hiyo inaona kuwa kuna hatari mbalimbali za ndani na nje ambazo zinaweza kudhoofisha hali ya uchumi.