Sudan Kusini kutoa vitalu vipya 14 vya mafuta kwa wawekezaji
2022-09-15 09:40:14| CRI

Mkurugenzi Mkuu wa Muungano wa Makampuni ya Mafuta ya serikali ya Sudan Kusini, Kampuni ya Nile Petroleum Corporation Limited (Nilepet), Bw. Chol Deng Thon Abel amesema kuwa Sudan Kusini itatoa vitalu vipya 14 vya mafuta kwa wawekezaji ili kuongeza uzalishaji hadi kufikia viwango vya kabla ya vita ambavyo ni mapipa 350,000 kwa siku.

Bw. Thon amesema hayo wakati wa kufungwa kwa mkutano wa 5 wa mafuta na nishati wa mwaka.

Bw. Thon ameongeza kuwa wana vitalu 14 vya mafuta ambavyo havijachukuliwa, hivyo wanakaribisha makampuni ya kimataifa kutumia fursa ya kuomba vitalu hivi, ambapo hivi sasa Sudan Kusini ina shughuli nyingi za kuvutia makampuni ya kimataifa kwenda kuwekeza kwenye sekta ya mafuta, na kusema mkutano huo ni jukwaa zuri sana la kubadilishana mawazo na makampuni ya kimataifa.