Rais Ruto akutana na mwakilishi maalumu wa serikali ya China anayeshughulikia mambo ya Afrika
2022-09-15 09:37:12| CRI

Rais wa Kenya William Ruto amekutana na mwakilishi maalumu wa serikali ya China anayeshughulikia mambo ya Afrika Liu Yuxi na kubadilishana maoni kuhusu uhusiano wa pande mbili na masuala mengine wanayoshughulikia kwa pamoja.

Akiwasilisha salamu za pongezi za rais Xi Jinping kwa rais Ruto, Bw. Liu amesema urafiki kati ya Kenya na China una historia ndefu, ambapo umepata maendeleo ya kasi na kuwa mfano kwa maendelo ya pamoja katika nchi zinazoendelea.

Naye rais Ruto amesema Kenya inaishukuru China kwa msaada wake wa dhati kwenye uchumi na maendeleo ya jamii nchini Kenya, na kuahidi kwamba iko tayari kuimarisha zaidi ushirikiano wao. Akiwa amepokea mwaliko kutoka Kenya, mwakilishi Liu ametembelea nchi hiyo kuanzia Septemba 11 hadi 13 na kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais Ruto.