Idadi ya abiria wanaotumia reli ya SGR nchini Kenya yaongezeka kwa asilimia 32.7 katika nusu ya kwanza ya mwaka huu
2022-09-16 08:42:01| CRI

Idadi ya abiria waliosafiri kwa Reli ya SGR ya Mombasa-Nairobi iliongezeka kwa asilimia 32.7 katika nusu ya kwanza ya mwaka huu ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, kufuatia kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi.

Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya (KNBS) ilisema reli hiyo iliyojengwa na China ilibeba abiria milioni 1.12 katika kipindi hicho, likiwa ni ongezeko kubwa kutoka 754,313 katika kipindi kama hicho mwaka wa 2021.

KNBS ilisema mwezi Aprili ulirekodi idadi kubwa zaidi ya abiria 264,119, ikifuatiwa na 228,353 mwezi Machi na 175,936 mwezi Mei.

Ongezeko la idadi ya abiria katika mwezi wa Aprili linaweza kuhusishwa na likizo ya Pasaka wakati Wakenya waliposafiri kwenda Pwani kwa ajili ya mapumziko huku shughuli za utalii zikiimarika baada ya kukwamishwa na COVID-19.