Benki ya Maendeleo ya Afrika kukusanya dola za kimarekani 13 kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
2022-09-19 08:54:19| CRI

Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Akinwumi Adesina amesema, benki hiyo imetoa nafasi kwa wafadhili wake kukusanya dola za kimarekani bilioni 13 ili kuunga mkono hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi barani Afrika.

Akihutubia  mkutano wa tatu wa kuongeza fedha za  Mfuko wa Maendeleo ya Afrika, Adesina amesema, kutokana na mfuko huo, wakulima milioni 20 watapata teknolojia zenye uwezo mkubwa zaidi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Amesema wakati mabadiliko ya tabianchi yanapoisumbua Afrika, mfuko huo utawasaidia wakulima kupata bima dhidi ya athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi

Pia ameongeza kuwa, kutokana na mfuko huo hekta milioni 1 za ardhi zilizoharibiwa zitafufuliwa, na watu zaidi ya milioni 9.6 watapata nishati mbadala.