UM wasema Wasomali milioni 1.1 wakimbia makazi yao kutokana na ukame mkali
2022-09-21 08:39:34| CRI

Idadi ya watu wanaokimbia makazi yao kutokana na changamoto zinazohusiana na ukame nchini Somalia imeongezeka na kufikia milioni 1.1 kati ya Januari mwaka jana na mwezi Agosti mwaka huu.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa Inayoratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema, watu 98,900 walikimbia makazi yao kutokana na ukame mwezi Agosti, ikiwa ni ongezeko la asilimia 18 ikilinganishwa na mwezi Julai.

Ofisi hiyo imesema, takwimu hizo mpya zimekuja wakati wenzi wa kibinadamu wakiongeza kwa kasi shughuli za kukabiliana na ukame, na kuwafikia watu milioni 5.3 walioathiriwa na ukame kwa kuwapa msaada na ulinzi mpaka kufikia mwisho wa mwezi Agosti.