Africa CDC yatoa wito wa kuimarisha ufuatiliaji na hatua za udhibiti wa Ebola nchini Uganda
2022-09-22 08:57:30| CRI

Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) kimetoa wito kwa mamlaka nchini Uganda kuongeza hatua za ufuatiliaji na udhibiti baada ya nchi hiyo kutangaza mlipuko wa ugonjwa wa Ebola kufuatia kuthibitishwa kwa kesi moja katika hospitali ya Rufaa ya Mubende.

Taarifa iliyotolewa na Kituo hicho imependekeza wilaya za jirani na zilizoathiriwa kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huo na vipimo vya maabara, na kutekeleza hatua sahihi za kuzuia maambukizi na udhibiti.

Pia Kituo hicho kimesema uchunguzi kuhusu chanzo cha maambukizi na watu waliowasiliana kwa karibu na mgonjwa unaendelea, ambapo ripoti za uchunguzi wa awali zimeonyesha kuwa, vifo sita katika vituo vya afya na hospitali katika wilaya hiyo havijafahamika chanzo chake.