Zimbabwe kuanza kusafirisha matunda aina ya machungwa kwenye soko la China
2022-09-30 09:20:47| CRI

Zimbabwe inatarajiwa kuanza kusafirisha matunda mabichi aina ya machungwa, kufuatia ukaguzi uliofanywa na idara ya forodha ya China.

Ofisa mwandamizi wa serikali ya Zimbabwe Bw. John Bhasera amesema kwa sasa Zimbabwe inakamilisha ripoti yake kuhusu hali baada ya ukaguzi huo ili kuikabidhi kwa China ndani ya siku chache.

Amesema kwa sasa Zimbabwe inapanga kusafirisha machungwa, malimao na mabalungi.

Idara ya kutangaza biashara ya Zimbabwe (ZimTrade) imekaribisha hatua hiyo, na kusema itapanua idadi na aina na bidhaa za Zimbabwe zinazouzwa nje ya nchi.