CMG yazindua vipindi maalum vya “Kufumbua Siri ya Maendeleo ya Miaka Kumi ya China” kwa lugha mbalimbali ndani na nje ya nchi
2022-09-30 14:46:45| CRI

Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG leo tarehe 30 hapa Beijing limefanya hafla ya kuzindua vipindi maalum vya “Kufumbua Siri ya Maendeleo ya Miaka Kumi ya China” kwa lugha mbalimbali ndani na nje ya nchi. Naibu mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC, mkuu na mhariri mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong alihudhuria hafla hiyo na kuzindua vipindi hivi maalum akiwa pamoja na wageni walioalikwa.

Kuanzia leo, vipindi hivi vitangazwa kwa Kiingereza, Kihispania, Kifaransa, Kiarabu na Kirusi kupitia televisheni ya CGTN. Tovuti kama vile ya CGTN, CRI Online, na CCTV, pamoja na akaunti za mitandao ya kijamii, zitarusha vipindi hivyo, na kukuza ushirikiano wa vyombo vya habari vya ng'ambo kutimiza utangazaji mpana.