Watumishi wa afya 65 nchini Uganda wawekwa karantini kutokana na virusi vya Ebola
2022-10-03 10:17:52| CRI

Msemaji wa Wizara ya Afya ya Uganda Bw. Emmanuel Ainebyoona amesema watumishi wa afya wasiopungua 65 nchini humo wamewekwa karantini kutokana na kuwa karibu na watu wenye virusi vya Ebola.

Ainebyoona amesema watumishi hao wa afya watakuwa nyumbani kwa siku 21, muda ambao hali yao ya afya itafuatiliwa. Pia amesisitiza kuwa hali imedhibitiwa.

Haya yanakuja baada ya daktari mmoja Mtanzania kufariki kwa Ebola siku ya Jumamosi katika wilaya ya Kabarole magharibi mwa Uganda.