Viongozi wa Somalia walaani shambulizi la bomu la kujitoa muhanga huku idadi ya vifo ikifikia 15
2022-10-04 10:02:39| CRI

Viongozi wa Somalia wamelaani mashambulizi mawili ya mabomu ya kujitoa muhanga yaliyotokea katika mji ulipo katikati ya Somalia wa Beledwyene, ambapo watu 15 wameuawa na wengine 26 kujeruhiwa.

Wakitoa taarifa kwa nyakati tofauti, rais Hassan Sheikh Mohamud na Waziri Mkuu Hamza Abdi Barre wameelekeza mashirika ya usalama kuchukua hatua zaidi za kupambana na ugaidi ili kuhakikisha usalama nchini humo.

Mohamud pia ametuma salamu za rambirambi kwa familia na ndugu wa watu waliopoteza maisha kwenye milipuko hiyo ambayo ililenga maafisa wa kituo cha Lamagalay ambacho ni makao makuu ya utawala wa mkoa wa HirShabelle. Ameiagiza serikali kuwatibu haraka watu wenye hali mahututi.