Mijadala miwili mikuu kufanyika wakati Gabon ikiwa mwenyekiti wa Baraza la Usalama la UM kwa mwezi Oktoba
2022-10-04 10:08:12| CRI

Gabon, nchi mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi Oktoba imesema mijadala miwili itakayoangazia “amani na usalama barani Afrika” na “hali ya hewa na usalama barani Afrika” itafanyika mwezi huu kwenye Baraza hilo.

Mwakilishi wa kudumu wa Gabon katika Umoja wa Mataifa na mwenyekiti wa Baraza la Usalama kwa mwezi Oktoba balozi Michel Xavier Biang amesema mjadala wa kwanza utalenga kuimarisha mapambano dhidi ya ufadhili wa makundi yenye silaha na magaidi kupitia usafirishaji haramu wa maliasili, na unatarajiwa kuendeshwa na Rais Ali Bongo Ondimba wa Gabon. Na mjadala mwingine unatarajiwa kuendeshwa na waziri wa mambo ya nje wa Gabon Michael Moussa-Adamo.

Baraza hilo pia limepanga kufanya mjadala wake wa kila mwaka kuhusu ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na mashirika ya kikanda.