China yazikosoa nchi zinazotekeleza sheria za kibaguzi dhidi ya kundi la watu wachache
2022-10-05 09:39:30| CRI

Mkuu wa Ujumbe wa China kwenye Umoja wa Mataifa mjini Geneva Chen Xu amesema japokuwa zaidi ya miaka miwili imepita tangu mmarekani mwenye asili ya Afrika George Floyd kufariki kutokana na matumizi ya nguvu ya polisi, utekelezaji wa sheria za kibaguzi dhidi ya kundi la watu wachache unaofanywa na idara za sheria, na ghasia na vifo vinavyohusiana na jambo hilo vinaendelea kuibuka katika baadhi ya nchi.

Akizungumza kwa niaba ya kundi la nchi katika kikao cha 51 kinachoendelea cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Chen alisema utekelezaji wa sheria ya ubaguzi wa rangi na ukatili ni masuala ya muda mrefu na kimfumo na yanakwenda sambamba na ukosefu wa usawa katika jamii za nchi hizi, na huu ni urithi wa utumwa na ukoloni katika historia zao.

Alisema kundi la watu wachache wakiwemo wale wenye asili ya Afrika, Asia na Waislamu katika nchi hizi, kwa muda mrefu wamekuwa wakibaguliwa na kutengwa huku haki zao zikikiukwa na usalama wao kukabiliwa na vitisho.