UM: Kambi ya walinda amani nchini DRC yashambuliwa kwa mara ya pili ndani ya wiki moja
2022-10-07 09:46:44| CRI

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa, kwa mara ya pili ndani ya wiki moja, wamezuia shambulizi kwenye kambi yao iliyopo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), baada ya wafuasi wanaoshukiwa kuwa wa kundi la wanamgambo wa Twirwaneho kushambulia Jumatano katika kambi ya Minembwe mkoa wa Kivu Kusini.

Kwa mujibu wa Stephane Dujarric, msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, askari wa kulinda amani walirejesha mashambulizi, ambapo waasi walilazimika kutawanyika, na kuongeza kuwa hakuna majeruhi kwa upande wa walinda amani.

Sambamba na hilo amesema mlinda amani kutoka Pakistan aliuawa kwenye shambulizi la Septemba 30, ambalo lililaaniwa vikali na Guterres. Kambi ya Minembwe ni sehemu ya Tume ya Umoja wa Matifa inayojiulikana kama MONUSCO.