Mtaalamu wa Nigeria: Mkutano mkuu wa 20 wa CPC wabeba matarajio ya dunia
2022-10-10 10:42:49| CRI

Mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) utakaofunguliwa rasmi Oktoba 16 mjini Beijing si kama tu ni jambo kubwa la China, bali pia utatoa athari za kina kwa dunia nzima. Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa China ya Nigeria Bw. Charles Onunaiju amesema, mkutano huo muhimu si kama tu unabeba matarajio ya watu wa China, bali pia unabeba matumaini ya dunia nzima. Mkutano huo ukiwa ni mwanzo mpya, dunia inaitarajia China kutimiza maendeleo zaidi na kutoa mchango mkubwa katika jumuiya ya kimataifa.

Alipohojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, Bw. Onunaiju amesema ameshuhudia mwenyewe maendeleo na mabadiliko makubwa yaliyotokea katika muongo uliopita tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC ufanyike. Amesema kila alipokuja China alijionea mabadiliko ya kushangaza, hasa wakati alipotembelea mikoa ya Shaanxi, Anhui, Tibet, Sichuan na Zhejiang, alishuhudia maendeleo makubwa kwenye maeneo ya vijijini, ambako wakulima wameondokana na umaskini na kuhamia kwenye nyumba mpya zenye mazingira bora ya kuishi. Anaona chama cha kikomunisti cha China kamwe haijabweteka na mafanikio kiliyoyapata, na siku zote kimekuwa kikiendeleza jitihada zake kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi. Dunia inatarajia kuwa mkutano mkuu wa 20 wa CPC utachochea zaidi msukumo wa ndani wa China wa kutimiza maendeleo.

Bw. Onunaiju pia anatarajia kuwa mkutano huo utaendelea kutoa ishara chanya katika kusukuma mbele maendeleo ya pamoja ya dunia nzima. Amesema katika miaka kumi iliyopita tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC ulipofanyika, China imetoa misaada mbalimbali halisi kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Afrika, akitolea mfano wa ushirikiano wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” ambao umefunika karibu bara zima la Afrika, kutia nguvu kubwa ya msukumo kwenye ushirikiano wa kunufaishana kati ya Afrika na China, na kutoa mwitikio mkubwa ambao haujawahi kutokea katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kihistoria zinazoikabili Afrika kama vile miundombinu. Amesema, miundombinu mingi ya sasa inayounganisha nchi za Afrika imejengwa chini ya mfumo wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na kutoa mchango mkubwa katika kuhimiza muunganiko na mafungamano ya kikanda katika bara la Afrika.