Syria yasema Marekani kuiba mafuta kutoka nchi hiyo ni kitendo cha 'uharamia'
2022-10-10 08:56:45| cri

Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imesema, kitendo cha Marekani kuiba mafuta ya nchi hiyo katika mpaka wa Syria na Iraq na kuyasafirisha hadi kaskazini mwa Iraq ni kitendo cha "uharamia" ambacho kimekiuka sheria za kimataifa na "Mkataba wa Umoja wa Mataifa".

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Mafuta na Rasilimali za Madini nchini Syria, kuanzia mwaka 2011 hadi katikati ya mwaka huu, uwepo wa jeshi la Marekani nchini Syria na uchimbaji madini na biashara haramu ya makundi yaliyoungwa mkono na jeshi la Marekani kumeisababishia Syria hasara za dola za kimarekani bilioni 107.1.