Timu ya madaktari ya China yatoa mafunzo ya huduma ya kwanza nchini Guinea
2022-10-11 08:42:57| cri

Timu ya 29 ya msaada wa matibabu za China nchini Guinea jana ilitoa mafunzo ya huduma ya kwanza katika Hospitali ya Urafiki ya China na Guinea mjini Conakry, nchini Guinea.

Timu hiyo ilitoa mazoezi na mafunzo kwa wafanyakazi wa matibabu wa hospitali hiyo kuhusu ufufuaji wa moyo na mapafu, huduma ya kwanza ya Heimlich, jinsi ya kuhamisha mgonjwa, na matibabu ya dharura.