Idadi ya vifo vilivyotokana na Ebola nchini Uganda yafikia17
2022-10-11 08:45:23| CRI

Msemaji wa Wizara ya Afya nchini Uganda Emmanuel Ainebyoona amesema, idadi ya vifo vilivyotokana na Ebola nchini humo imeongezeka na kufikia 17 kutoka 10 ilivyoandikishwa siku mbili zilizopita.

Pia amesema hadi kufikia tarehe 9 Oktoba, kesi 48 zimethibitishwa baada ya kesi 4 mpya zilizosajiliwa katika saa 48 zilizopita, na kati ya kesi hizo, tisa ni wafanyakazi wa afya, na 14 wamepona.  

Mapema jana, Ainebyoona alithibitisha kuwa timu ya maafisa wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ilikuwa nchini humo kujadiliana namna ya kukabiliana na Ebola.

Kwa mujibu wa WHO, maofisa waandamizi pia watahudhuria Mkutano wa dharura wa mawaziri kuhusu ushirikiano wa kuvuka mipaka ya nchi ili kukabiliana na ugonjwa wa Ebola utakaofanyika tarehe 12 Oktoba.