Ethiopia yatimiza maendeleo ya uchumi na jamii licha ya changamoto zilizopo
2022-10-12 08:23:59| CRI

Rais wa Ethiopia Sahle-Work Zewdw amesema, nchi hiyo imepata maendeleo ya kiuchumi na kijamii licha ya changamoto zinazosababishwa na binadamu na majanga ya kimaumbile.

Akizungumza katika kikao cha pamoja cha Bunge la Chini pamoja na Baraza la Juu la Bunge la Ethiopia jana jumanne, rais Zewdw amesema matokeo yaliyopatikana katika sekta ya uchumi na jamii yanaonyesha kuwa serikali imetekeleza kikamilifu sera zilizosaidia kumudu ukosefu wa utulivu wa uchumi duniani.

Pia Rais Zewsw amesisitiza kuwa, maendeleo ya uchumi na jamii yamepatikana licha ya changamoto zinazoendelea kutokana na mapigano nchini humo, ukame, mafuriko na pia ukosefu wa utulivu wa uchumi wa dunia.