Mawaziri wa afya wa Afrika wakutana na kujadiliana mlipuko wa Ebola nchini Uganda
2022-10-13 08:26:42| CRI

Mawaziri wa afya kutoka nchi 11 za Afrika wamekutana Jumatano nchini Uganda ili kujadiliana kuhusu ugonjwa wa Ebola ulioibuka hivi karibuni nchini humo.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Uganda, mawaziri hao wanajadili ushirikiano wa kuvuka mipaka ili kujiandaa na kukabiliana na Ebola.

Wizara ya Afya ya Uganda ambayo ni nchi mwenyekiti mwenza na Umoja wa Afrika, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika, na WHO, wamesema mkutano huo utaimarisha ushirikiano katika kukabiliana na homa ya hemorrhagic na hali nyingine dharura za afya ya umma.