China yahimiza nchi zilizoendelea kutimiza ahadi yao ya kuisaidia Afrika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
2022-10-13 10:12:18| CRI

Naibu mwakilishi wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing amehimiza nchi zilizoendelea kutimiza ahadi yao ya kuzisaidia nchi za Afrika kupata fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi haraka iwezekanavyo.

Balozi Dai amesema hayo kwenye majadiliano ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa na usalama barani Afrika. Amesisitiza kuwa, kuisaidia Afrika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi si ahadi ya maneno matupu, na nchi zilizoendelea zinapaswa kutimiza ahadi yao, na kuitikia mahitaji ya nchi za Afrika.

Balozi Dai amesema jambo muhimu ni kuisaidia Afrika kuimarisha uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na kuharakisha kusukuma mbele ajenda ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030.