Uganda yatangaza hatua za zuio katika wilaya zilizoathiriwa na Ebola
2022-10-17 09:08:41| CRI

Rais Yoweri Museveni wa Uganda ametangaza uamuzi wa kuweka karantini mara moja kwenye wilaya Mubende na Kassanda kutokana na janga la Ebola.

Akihutubia kwa njia ya televisheni, Rais Museveni amesema hatua za zuio zitatekelezwa kwa muda wa siku 21, na katika kipindi hicho hakuna atakayeruhusiwa kuingia au kutoka katika wilaya hizo.

Sambamba na hatua hizo mikusanyiko yote ya umma ya ibada na burudani imepigwa marufuku, lakini shule zitaendelea kufunguliwa chini ya usimamizi mkali wa maofisa wa afya.

Wilaya ya Mubende ndio kiini cha mlipuko wa sasa wa  ugonjwa huo ambao hadi sasa umeambukiza watu 58, watu 19 kati yao wamefariki dunia na wengine 20 wamepona.