China kuhimiza kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja na kukuza thamani ya pamoja ya binadamu
2022-10-17 16:19:44| cri

Mkutano Mkuu wa 20 wa Wajumbe Wote wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambacho ni chama tawala cha China umefunguliwa tarehe 16 mjini Beijing. Xi Jinping alitoa hotuba kwenye mkutano huo kwa niaba ya kamati kuu ya 19 ya CPC akisema, siku zote China inashikilia kanuni ya sera ya kidiplomasia juu ya kulinda amani ya dunia na kuhimiza maendeleo ya pamoja, na inadhamiria kuhimiza kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja na kutoa wito kwa nchi mbalimbali duniani zikuze thamani ya pamoja ya binadamu ikiwa ni pamoja na amani, maendeleo, usawa, haki, demokrasia na uhuru.

Xi amesema mabadiliko makubwa yanatokea hivi sasa. Kwa upande mmoja, wimbi la historia lenye amani, maendeleo, ushirikiano na kunufaishana halitazuiliwa, na kwa upande mwingine, kitendo cha umwamba kina madhara makubwa.

Xi amesisitiza tena kuwa China inafuata sera za kidiplomasia ambazo ni huria, za kujiamulia na za amani. Siku zote China inaamua msimamo na sera zake kulingana na hali halisi, kulinda kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa na usawa na haki duniani, na inapinga kithabiti aina yoyote ya umwamba na siasa za kimabavu, pia inapinga wazo la Vita Baridi, vitendo vya kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine, na kupinga vigezo viwili. China haitafanya umwamba, wala haitavamia nchi nyingine daima.

Xi amesema China inashikilia kanuni ya kimsingi ya kufungua mlango kwa nje, kushikilia kithabiti mkakati wa kufungua mlango wenye kunufaishana, kuhimiza uhuru na urahisi wa biashara na uwekezaji, kuhimiza ushirikiano wa pande mbili, kikanda na pande nyingi, na kuhimiza uratibu wa sera ya hali ya jumla ya uchumi. China inapinga sera ya kujilinda, vikwazo vya upande mmoja na kuweka shinikizo kupita kiasi. Pia China inapenda kuongeza uwekezaji wa rasilimali katika ushirikiano wa maendeleo ya dunia, kupunguza pengo kati ya nchi za Kaskazini na Kusini, kuunga mkono na kusaidia kithabiti kuharakisha maendeleo ya nchi zinazoendelea.